AdSense

Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Thursday, 9 April 2015

On 21:30 by Unknown in    No comments
shambulizi Milan 
 
Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.
Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.
Shambulizi la Milan 
 
Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake.
Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Maafisa wa polisi mjini Milan baada ya shambulio la mahakamani 
 
Mshukiwa huyo alikamatwa kaskazini mwa Milan akitoroka kwa pikipiki.
Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.

On 21:27 by Unknown in    No comments
 
Wakimbizi wa Palestina 
 
Raia wa Palestina wanasema kuwa wamekubali kushirikiana na serikali ya Syria ili kujaribu kuwafurusha wapiganaji wa IS nje ya kambi moja ya wakimbizi viungani mwa Damascus.
Tangazo hilo hilo lilifanywa na afisa mmoja wa serikali ya Palestina huko West Bank.
Wapiganaji wa IS walitekeleza shambulizi katika kambi hiyo wiki iliopita na kuweza kuiyumbisha kanbi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa jeshi la Palestina.
Takriban wakimbizi elfu kumi na nane wanaishi katika kambi hiyo ambayo inakabiliwa upungufu mkubwa wa vitu muhimu.

On 21:19 by Unknown in    No comments
 
Je unataka Kuwa Mrembo na Muonekano wa Kupendeza kwa Kuongeza Hips, Makalio, Mapaja, Kurefusha Nywele, Kupunguza Unene na Kuondoa Tumbo? Basi African Beauty Products Wanakuletea Hii:
Kabla ya Kutumia Dawa na Baada ya Kutumia Dawa zetu
1.Kuongeza Hips Makalio na Mapaja 100,000/
2.Kunenepesha Miguu iwe chupa ya Bia 70,000/
3.Kuwa Mnene Mwili Mzima 80,000/
4.Kupunguza Tumbo na Nyama Uzembe 80,000/
5.Kupunguza ama Kuongeza Maziwa 60,000/
6.Kuwa Mweupe na Soft Mwili Mzima 100,000/
7.Kuondoa Chunusi na Madoa 60,000/
8.Kuondoa Michirizi na Mabaka 70,000/
9.Kupunguza Unene Mwili Mzima  80,000/
10.Kuongeza urefu na unene wa Uume 90,000/
 
Bidhaa Zetu ni Uhakika Matokeo  Ndani ya Week Moja..
Tuwasiliane kwa Simu Namba:
0756697906 ,0716805391 au 0783300397
 
Kwa watu wa Dar es Salaam Utaletewa Popote Ulipo ..Kwa Watu wa Mikoani tunatuma kwa Basi

Monday, 6 April 2015

On 05:26 by Unknown in    No comments
Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 255 CRN na lililokuwa na Tela lenye namba za usajili T 478 BCG likiwa limefunga njia baada ya kufeli breki lilipo kuwa kwenye njia kubwa katika eneo la Mbezi Mwisho, Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Dereva wa Lori hilo aliejitambulisha kwa jina moja la Bw. Sendegwa, alisema kuwa alianza safari yake ya kutoka Mkoani Singida akiwa vizuri kabisa na alipofika maendeo ya Kibamba alihisi gari yake kupoteza upepo lakini kwa wakati huo alikuwa kwenye mwendo mdogo tayari na alianza kujarubu kutafuta namna ya kusimama lakini hakufanikiwa, na alipofika maeneo ya Mbezi aliona sehemu ya kuchepuka ambayo aliona ni salama kwa upande wake na ndipo alipoamua hivyo na huko alikutana na Gari dogo aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 902 DCS ambapo alilipiga pasi ubavuni na kwenda kukita kwenye baraza la moja ya nyumba zilizokuwepo kwenye eneo hilo.
Hakuna aliejeruhiwa wala kupoteza maisha kwenye ajali hiyo. 
Lori hilo linavyoonekana baada ya kufeli breki na kuja kusimama hapo. 
 
Muonekano wa Prado hiyo baada ya kupigwa pasi na Lori hilo. 
 
Dereva wa Prado hiyo (jina kapuni) akijadiliana jambo na utingo wa Lori hilo. 
 
Mashuhuda wakiangalia namna Prado hiyo ilivyopigwa pasi. 
 
Neno la Leo lililoandikwa kwenye Lori hilo. 
 
Mashuhuda wakihadithiana namna mambo yalivyokuwa. 
 
Hapa ndipo Lori hilo lilipogota. 
 
On 05:23 by Unknown in    No comments
 
Matukio ya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, vikongwe na watu wa makundi mengine ya kijamii nchini, yametajwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na hofu na kutojiamini kwa baadhi ya watu, hivyo kujikuta wakitumia nguvu za ziada kutaka kufanikisha mambo yao, badala ya kumtegemea Mungu.
 
Hayo yamebainishwa kwenye Ibada ya Sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front na Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Dk Alex Malasusa.
 
Alisema hofu na kukosa uhakika ni chanzo kikubwa cha dhambi jambo ambalo linawafanya watu kuingia katika matendo ya ushirikina na mauaji ya binadamu wenzao.
 
“Watu wengi wamekuwa wakishiriki ushirikina na si kwamba wanapenda ushirikina, hawapendi, lakini wamejawa na hofu na hawana uhakika na ndio chanzo cha dhambi. Kumekuwapo na matukio mengi ya ushirikina ambayo si kawaida kwa binadamu aliyeumbwa na akili akayatenda."
 
Malasusa aliongeza: “Haijalishi umesoma kiasi gani, leo hii imethibitika wasomi wengi wameingia kwenye ushirikina, haijalishi una hali gani ya kiuchumi, wafanyabiashara wengi wamejiingiza kwenye ushirikina, haijalishi unapenda ibada kiasi gani, imethibitika tunaoingia na kutoka ibadani bado tunashiriki ushirikina.
 
“Ndio maana tunasikia matendo ya kusikitisha ya binadamu kwenda kuua binadamu wenzao kama albino, vikongwe kutokana na kujawa na hofu, eti wanaamini kwa kuua albino watapata fedha au mafanikio kwenye uchaguzi, huo ni uovu na akili za kishetani. Yesu aliyefufuka ndio atakayekupa mafanikio.”
On 05:20 by Unknown in    No comments
 
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alihubiri akiwa katika kiti cha magurudumu na kusema hawezi kuwatupa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi. 
 
Pia askofu huyo, amewataka waumini wote wa kanisa hilo kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi, Alhamisi ijayo siku ambayo atakwenda kukamilisha mahojiano dhidi ya tuhuma za kumtukana Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.
 
Akihubiri mamia ya waumini waliofika kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Pasaka jana, Gwajima alisema kumekuwa na uvumi kwamba kuhojiwa kwake na polisi kulitokana na kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa nyakati tofauti na kuzungumza na waumini wake.
 
Alisema alifahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 wakati huo mbunge huyo akiwa Waziri wa Ardhi na tangu kipindi hicho amekuwa mtu wake wa karibu.
 
Alisema alifahamiana na Dk Slaa tangu mwaka 1994 kabla hajagombea nafasi ya urais kupitia Chadema na kwamba tangu wakati huo amekuwa rafiki wa familia.
 
“Hawawezi kunichagulia marafiki, hawa ni watu wangu wa karibu hata kabla hawajawa na ndoto za kugombea urais, nitaendelea kuwa nao karibu,” alisema.
 
Asimulia mahojiano
Akizungumzia mahojiano yake na polisi, Gwajima aliwaeleza waumini wake kwamba mambo mengi aliyohojiwa hayakuhusiana na suala la kumkashifu Kardinali Pengo.
 
“Polisi walinihoji mambo mengi binafsi yanayonihusu mimi na hayakuhusiana kabisa na Pengo, maswali ya Pengo yalikuwa machache sana,” alisema.
 
Hata hivyo, Gwajima alisema hana ugomvi na polisi wala Serikali kwa kuwa amekuwa akitoa ushirikiano kwa vyombo hivyo. Akitoa mfano, alisema Februari mwaka huu alipeleka barua polisi kueleza anataka kudhamini kampeni kwa ajili ya kupinga mauaji ya albino kwa kushirikiana na jeshi hilo.
 
“Niliwaeleza kwamba tungezunguka na polisi mikoa yote Tanzania na wamenijibu kwamba nipeleke ratiba ya shughuli hiyo ili tuanze,” alisema.
 
Alisema pia alidhamini mafunzo ya ulinzi shirikishi kwa vijana 400 kwa kushirikiana na polisi... “Shughuli hizi zinaonyesha kwamba sina ugomvi na polisi, bali nimekuwa rafiki kwa kushiriki katika shughuli zenye masilahi kwa Taifa.”

Viongozi wamiminika
Alisema pia hana ugomvi na Serikali na kwamba viongozi wake wamekuwa wakimiminika katika kanisa lake.
 
Aliwataja viongozi hao kuwa ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe.
 
Viongozi wengine, alisema ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee na wabunge wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa na Vicky Kamata wote wa CCM 
  
 “Kama ningekuwa na ugomvi na Serikali viongozi hawa wasingekuja katika kanisa langu kwa nyakati tofauti. Hii inaonyesha nilivyo na uhusiano mzuri na Serikali,” alisema.
 
Alhamisi ijayo
Askofu Gwajima amewataka waumini wake kumsindikiza katika Kituo cha Polisi siku ambayo atahojiwa kwa mara nyingine. “Nitakwenda Central Police Alhamisi saa moja asubuhi, nawaomba waumini wote mfike katika eneo hilo lakini msilete fujo wala kumtukana mtu, kuweni watulivu wakati wote nitakapokuwa nahojiwa,” alisema.
 
Askofu huyo alitakiwa kuhojiwa Alhamisi iliyopita lakini polisi waliahirisha kutokana na hali yake kutokuwa ya kuridhisha.
 
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Jeshi la Polisi halitaruhusu mkusanyiko wa watu katika eneo hilo wakati Askofu Gwajima atakapohojiwa.
 
“Atatakiwa kufika na wakili wake na mtu mmoja ambaye ataona anafaa kuingia naye kwenye mahojiano. Kama kuna waumini wanajiandaa kukusanyika katika ofisi zetu hapa Central Polisi, wafahamu kwamba haturuhusu na wakikaidi tutachukua hatua.”
 
Ilivyokuwa kanisani
Gwajima alifika katika kanisa hilo lililopo kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe saa 5.00 asubuhi na kupokewa kwa shangwe na waumini walioanza kufika tangu saa 2.00 asubuhi.
 
Msafara wa magari matatu; Toyota Land Cruiser mbili na Hammer, yaliwasili kwenye viwanja vya kanisa hilo na kulakiwa na waumini walioyazingira kwa shangwe na vigelegele wakitaka kumwona Askofu Gwajima.

Waumini hao walikuwa na shauku ya kumwona Gwajima na walionekana wakisukumana ovyo kila mmoja akitaka kumwona.
 
Akiwa amevaa suti ya rangi ya kijivu na shati jekundu, Gwajima aliteremka katika Hammer akishikiliwa na wasaidizi wake na kukalishwa katika kiti cha magurudumu mawili kilichokuwa kikisukumwa na wasaidizi hao kuelekea kwenye jukwaa la kanisa hilo.
 
Baada ya kufika, vikundi vya kwaya viliendelea kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali za kumtukuza Mungu.
 
Gwajima alizungumza na waumini wake kuanzia saa 5.30 hadi saa 6.45, akiwaeleza kilichotokea kuanzia siku alipofika polisi kwa mara kwanza, mahojiano hadi alipotoka hospitali.
 
Katika mahubiri yake, Gwajima alisema ataendelea kuwaonya viongozi wa Serikali na wa dini watakaokosea masuala mbalimbali.
  

 “Sitajali ni kiongozi wa aina gani amekosea nitawakemea. Rais akikosea nitamkemea. Waziri akikosea nitamkemea na viongozi wa dini wakikosea nitaendelea kuwakemea,” alisema.

On 05:13 by Unknown in    No comments
 
Mahmoud Abbas 

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amekataa kukubali mamilioni ya dola ambazo ni fedha za kodi ambazo zilikuwa zimezuiliwa na Israeli.
Bwana Abbas alisema kuwa aliamua kurudisha pesa hizo kwa sababu Israeli ilikuwa imekata kiasi fulani ili kulipa kile ilichosema kuwa ni madeni kwa makampuni ya nchi yake.
Bwana Abbas alisema kuwa pesa zilizokatwa ni kama thuluthi moja ya pesa zote ambazo Israeli imekuwa ikizuia.
Amesema kuwa iwapo Israeli itakosa kulipa fedha zote hizo atapeleka kesi katika mahakama ya haki ya kimataifa ICC.
On 05:08 by Unknown in    No comments
 
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita.
Amisom 
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

Sunday, 5 April 2015

On 19:37 by Unknown in    No comments
 
Rais wa Somalia 

Mamlaka nchini Somalia imevifunga vituo viwili vya redio nchini humo baada ya kutangaza habari za wapiganaji wa Al-shabaab kuhusu shambulio la chuo kikuu nchini Kenya.
Kituo cha redio cha Sky FM na kile cha Shebelle vilifungwa huku mtangazaji na mkurugenzi wakikamatwa.
Vikosi vya usalama nchini Somali vimekuwa vikiwakamata wanahabari ambao hufanya mahojiano na wapiganaji wa Al-shabaab ama kutangaza habari zao.
On 19:34 by Unknown in    No comments
 
Ibada katika kanisa moja la Kianglikana nchini Kenya ilikatizwa ghafla baada ya tishio la ugaidi siku ya Jumapili.
Waumini walihamishwa kutoka kanisani hilo baada ya gari moja kuingia ndani ya uwanja wa kanisa kimabavu.
Kenya iko katika hali ya tahadhari baada ya mauaji ya watu wasiopungua 150 kaskazini mwa taifa taifa hilo.
Ibada hiyo ya Pasaka iligeuka na kuwa mbio za mguu niponye baada ya waumini kuarifiwa kuhusu gari hilo lisilo na nia njema.
Askofu wa kanisa hilo, Julius Kalu, amesema aliarifiwa kuhusu gari ambalo liliingizwa ndani ya uwanja wa kanisa bila hilo idhini kabla ya kusimamishwa kwenye lango kuu la kanisa lenyewe.
Askofu Kalu amesema waliokuwa ndani ya gari hilo walitoroka
Polisi waliitwa, na baada ya kulikagua gari hilo walilivuta hadi makao makuu ya polisi.
Mkuu wa polisi eneo la Mombasa Robert Kitur amesema hawakupata kitu, lakini wamelizuia gari hilo kwa uchunguzi zaidi.

On 19:25 by Unknown in    No comments
 
Katika maadhimisho ya ibada ya sikukuu ya Pasaka, baada ya mateso,kifo na ufufuko wa Yesu Kristo,Baba Mtakatifu Francis amewaombea wanafunzi waliouawa nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika utaratibu wake wa kawaida wa kutoa ujumbe katika sikukuu ya pasaka,akizungumza na umati wa waumini waliofurika katika viwanja vya Basilica ya Mtakatifu Peter mjini Vatican, Papa ametoa mwito wa kusitisha kile alichokiita matukio mengi ya mateso ya wakristo ulimwenguni.
Kiongozi huyo wa kiroho anayeongoza waumini wa madhehebu ya kikatoliki wapatao bilioni moja nukta mbili ,amelaani mgogoro unaondelea Mashariki ya kati na kwingineko, lakini ameweka imani yake katika mazungumzo yanayoendelea juu ya mkataba wa vinu vya nyukilia vya Irani ,wenye mwanga wa matumaini wa kufikiwa makubaliano na kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi.
Kabla ya kuanza hotuba yake,Papa alikwenda katika viwanja hivyo vya Basilica la Mtakatifu Petro kuwasalimia waumini waliokuwa wakimsubiri pamoja na kwamba kulikuwa na hali mbaya ya hewa.

On 19:23 by Unknown in    No comments
 
Serikali ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa watu wanne walioshambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya alhamisi na kuwaua watu 148.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazkazini mashariki mwa kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab.

Saturday, 4 April 2015

On 03:19 by Unknown in    No comments
 
Machi 31 mwaka huu, mwanamke mmoja mkazi wa Bwai wilayani Butiama, Kudra Nanja alifanyiwa ukatili na mumewe wa kuchomewa ndani ya nyumba kwa petroli, tukio lililosababisha mtoto wake Tatu Simioni aliyekuwa na umri wa mwezi mmoja na nusu kufariki dunia.
On 03:15 by Unknown in    No comments
 
Mahojiano baina ya Jeshi la Polisi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima yaliyokuwa yanatarajiwa kuendelea jana, ikiwa ni siku mbili baada ya kuachiwa kwa dhamana na jeshi hilo, jana yalikwama kuendelea kutokana na kile kilichoelezwa kutoimarika kwa afya ya askofu huyo, na sasa yatafanyika Alhamisi ijayo.

Gwajima alidaiwa kuzimia wakati akihojiwa na makachero wa Polisi waliokuwa wanamhoji, alipojisalimisha alasiri ya Ijumaa iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo, kutokana na kufunguliwa jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.
 
Kutokana na hali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu usiku wakati akiendelea na mahojiano yaliyoanzia alasiri, alikimbizwa Hospitali ya TMJ, Mikocheni akiwa chini ya ulinzi wa Polisi hadi aliporuhusiwa kutoka Jumanne wiki hii na baadaye kuachiwa kwa dhamana.
 
Mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alithibitisha kuahirishwa kwa mahojiano kati ya mteja wake na Polisi, akisema mapema jana asubuhi aliripoti Kikuo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyotakiwa kuripoti kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.
 
Hata hivyo, alisema hakuweza kuhojiwa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa afya ya mteja wake haijaimarika vizuri na hivyo wamepangiwa kurudi tena kituoni hapo Aprili 9 mwaka huu, yaani Alhamisi ijayo kwa ajili ya mahojiano.
 
“Mteja wangu alifika kituoni leo (jana) asubuhi kwa ajili ya mahojiano na pia kuripoti kama ilivyoagizwa siku alipopatiwa dhamana, hata hivyo afya yake bado haijaimarika na hivyo imewalazimu polisi wampatie muda zaidi hadi Aprili 9 atakaporudi tena kwa ajili ya mahojiano,” alisema Mallya.
 
Hata hivyo, Mallya alisema hali ya afya ya Gwajima imeanza kuimarika na kadri siku zinavyozidi kwenda, atakuwa na nguvu na ataendelea na kazi zake kama kawaida.
 
Mtumishi huyo alipatiwa dhamana katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kati kwa ajili ya mahojiano zaidi na kusubiri uchunguzi wa kesi yake ukamilike.

On 03:14 by Unknown in    No comments
 

Majaliwa ya kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu  Nchini , Shehe Ponda Issa Ponda, ambayo  ipo kwenye hatua ya utetezi itapatikana miezi mitatu ijayo.

Hiyo inatokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo Hakimu Mwandamizi wa Mahakama  hiyo, Mary Moyo kuanza rasmi likizo  ya uzazi ya miezi mitatu na hivyo Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Morogoro Maua Hamduni kuiahirisha  hadi Aprili 16, mwaka huu ambapo itatajwa tena mahakamani hapo.
 
Mtuhumiwa  alifikishwa mahakamani hapo pasipo mawakili wake wa utetezi , ambapo kwa jana  upande wa mashtaka uliongozwa  na Wakili wa Serikali, Sunday Hyera. 
 
Kabla ya kuanza kutoa maelezo ya kuahirishwa kwa kesi,  Hakimu huyo  alimuuliza Shehe Ponda juu ya kutoonekana kwa mawakili wake mahakamani hapo na endapo  anazo taarifa zao , naye  alijibu kuwa hakuwa na taarifa zao.
 
Kesi hiyo kwa sasa ipo katika  hatua ya upande wa mashtaka kujibu hoja zilizotolewa na upande wa utetezi baada ya kufungwa kwa ushahidi ambazo zilidai kuwa Shehe Ponda hakuwa na kesi ya kujibu.
 
Kutokana na hatua ilipofikiwa , Hakimu huyo, alisema  pamoja na  Hakimu Moyo anayeisikiliza kesi hiyo tangu mwanzo kuwa katika mapumziko ya likizo ya uzazi ya miezi mitatu, kisheria  haiwezekani shauri hilo ikabadilishiwa hakimu mwingine bali itaendelezwa naye baada ya kumaliza likizo ya uzazi.
 
Kwa mujibu wa Hakimu huyo, kwa hivi sasa kesi ya Shehe Ponda itaendelea kutajwa mahakamani hapo hadi hakimu wake atakapoanza kazi baada ya kumaliza likizo hiyo .
 
Kufuatia maamuzi ya hakimu huyo, Shehe Ponda alinyosha kidole mbele ya hakimu huyo na kupewa nafasi ya kuzungumza ambapo alimwambia hakimu kuwa kwa vile kesi yake itakuwa ikitajwa pekee, anaomba siku ya kufikishwa mahakamani abakie magereza ili kuondoa usumbufu.
 
Shehe Ponda alidai kuwa, ingekuwa ni jambo nzuri siku ya kutajwa kwa kesi yake iitwe fomu yake na kugongwa muhuri wa Mahakama , wakati akiwa gerezani .
 
Hata hivyo hakimu huyo alimjibu Shehe Ponda kuwa, kisheria njia hiyo hairuhusiwi , kwani kinachozingatiwa ni kwa mtuhumiwa kufikishwa mahakamani na hakimu kumwona kwa macho yake na kuiahirisha kwa msingi huo na si vinginevyo.
 
Hakimu huyo alimuuliza Sheikh Ponda kuwa yeye haoni kuwa ni fursa kuja uraiani kuonana  na kusalimiana na ndugu zake na kujibiwa na Sheikh Ponda kuwa, yeye amezoea kukaa gerezani hivyo haoni sababu hizo.
 
Tofauti na siku nyingine inaposikilizwa kesi hiyo ambapo wafuasi wake hufurika nje ya uzio wa mahakama hiyo , jana, walijitokeza wachache hawakuzidi  watu 10 ambao hawakuweza  kufanya jambo lolote  la kusoma Quraan na kufanya maombi .
 
Shekhe Ponda alifunguliwa kesi namba 128/2013 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo aliyatenda Augosti 10, mwaka 2013 katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro na alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 19 mwaka 2013.
On 03:05 by Unknown in    No comments
Wanawake wa mjini wanasema makubwa, madogo yana nafuu! Msemo huo unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Rukia Mabeseni mkazi wa Kigogo jijini Dar kukodi ngoma ya kibao kata kwa lengo la kwenda kumsuta shoga yake aitwaye mama Mariam.
 Rukia Mabeseni akimsuta shoga yake pamoja na wenzie.
Ilikuwaje? Msikie Rukia Mabeseni
“Shost wangu, huyu mama Mariam huyu aliwahi kumzawadia mwanangu baiskeli katika sherehe yake ya kuzaliwa, nikashukuru na nikajua shoga ninaye.“Cha ajabu juzijuzi hapa alikuwa na sherehe yake, bahati mbaya mimi sikuwa kwenye hali nzuri, nikampelekea zawadi ndogo, hee! Kumbe mwenzangu hajaridhika.

“Si akaanza kunisema vibaya kwa watu, eti kama hali yangu ilikuwa mbaya kwa nini sikusema mapema badala ya kumpelekea matambara, kwa kweli iliniuma sana.“Ndiyo nimeamua kumrudishia zawadi yake ya baiskeli kwa staili hii ili aweke kumbukumbu kuwa alichonifanyia si kitu kizuri,”  alisema Rukia.
 Wakizidi kumsuta.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwa eneo la tukio, Rukia akiwa na wapambe wake waliokuwa wamevalia sare za madera kufika nyumba kwa mama Mariam, hakufungua mlango kwa kukwepa aibu.Ikaelezwa kuwa, baada ya kundi hilo la wanawake lililokuwa likicheza kwa staili ya kukata mauno kuondoka, msutwaji huyo aliamua kukimbilia Kituo cha Polisi cha Kigogo kutoa taarifa akihisi kuwa watamrudia tena na kumfanyia vurugu.

Hata hivyo, baada ya Rukia kusikia kuwa wameenda kushitakiwa, walirudi tena ambapo safari hii mama Mariam alikubali yaishe kwa kuomba msamaha. “Ameomba msamaha na amefuta kesi kwa sababu alisema kuwa alighafirika tu, hata hivyo alinipigia simu na kuniambia anaumwa anaomba tuongee yaishe ikibidi tukamuone tumalize tofauti zetu,” alisema Rukia.

Thursday, 2 April 2015

On 03:55 by Unknown in    No comments
Ligue 1 giants Paris Saint Germaine are reportedly lining up a sensational bid for struggling Manchester United winger Angel di Maria, in the summer.

The Argentine international, who joined the Red Devils in a British transfer record last summer from Real Madrid, has struggled to adapt to the English game.

The Parisians were keen to sign the 27-year old last summer but the move fell through due to the Financial Fair Play regulations before he moved to Old Trafford in a staggering £59.7m deal.

The Premier League’s most expensive signing has not lived up to expectations at Old Trafford and it is suggested that United are ready to cut their losses at the end of the season.

United manager Louis van Gaal recently admitted that he has no guarantee that Di Maria will be at Old Trafford next season.

Speaking to reporters, the Dutch tactician said:  "As a manager, you can never say 'yes' or 'no' because the player shall always decide at the end. 

The Parisians are reportedly ready to test United’s resolve to keep the attacker with a £60m bid.
On 03:21 by Unknown in    No comments
 
Bei za mazao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu  za Pasaka katika soko la Kariakoo zimeongezeka kutokana na imani iliyojengeka kwa wafanya biashara kuwa uwezo wa manunuzi unakuwa juu.

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Florens Seiya alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
 
Seiya alisema kila inapofikia kipindi cha sikukuu kubwa za kidini, imekuwepo desturi kwa wafanyabiashara nchini kupandisha bei za vitu sio kwenye bidhaa tu hata nguo ama usafiri.
 
Alitaja bidhaa zinazopanda bei katika kipindi hiki kuwa ni nyanya maji, vitunguu maji, pilipili hoho, vitunguu swaumu, tangawizi, karoti, njegere, matunda mbalimbali na mchele. Alisema wastani wa ongezeko za bei hizo ni Sh 5,000 hadi 100,000 kutokana na aina ya  mazao.
 
Alitolea mfano nyanya kwa kawaida hivi sasa boksi ni Sh 35,000 lakini kipindi hiki imekuwa Sh 40,000. Mchele gunia ni Sh 150,000 kipindi cha sikukuu ni Sh 200,000. Tangawizi awali gunia liliuzwa Sh 200,000 hivi sasa ni Sh 300,000.
On 03:18 by Unknown in    No comments
 
Licha ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya.


Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa hospitali ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu kwa dakika 15 juzi, Mbasha alisema: “Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine.
 
“Mimi ndoa yangu haipo,  mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?”

Mbasha alikwenda mbele zaidi kwa kutoa tamko na agizo kwa mchungaji huyo kwa kusema:
 
“Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha.
 
“Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye asiwe na kinyongo na mimi.”
 
Mbasha hakumalizia hapo, alipoulizwa kama kauli ya Gwajima iliyosababisha mtafaruku ilikuwa sawasawa au la! Mbasha alisema:
 
“Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe msamaha.”
 
Naye mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alipopatikana kwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya Mbasha, alisema: 
 
“Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.
 
“Gwajima na Flora hawana uhusiano wowote usiofaa. Sasa yeye anaposema kalipiwa, kalipiwa kitu gani? Mungu anaweza kulipa jambo la hisia?”

Wiki mbili zilizopita, kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkers ambako kuna kanisa,  Gwajima alitoa mahubiri yaliyolenga kumshutumu Kadinali Pengo kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Maaskofu Tanzania kuhusu msimamo wao wa Mahakama ya Kadhi nchini.
 
Hali hiyo ilimfanya Gwajima kuitwa Polisi Kituo cha Kati, Dar na kuhojiwa. Akiwa katika mahojiano, ghafla alisikia kizunguzungu, akaanguka na kupoteza fahamu. alikimbizwa katika Hospitali ya Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.
 
Juzi, Gwajima aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo lakini akachukuliwa hadi Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi na kuachiwa kwa dhamana.

On 03:17 by Unknown in    No comments
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa hati ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma anayekabiliwa na kesi ya kupokea Sh milioni 323.4, kwa kuwa hajafika mahakamani.

Aidha imetoa hati kwa wadhamini wa Mujunangoma kufika mahakamani kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kutokana na kitendo chao na mshitakiwa kutofika mahakamani.
 
Hakimu Mkazi Emmilius Mchauru alitoa hati hizo jana wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa ajili ya kusikiliza pingamizi, lililowasilishwa na upande wa utetezi.
 
Awali, Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliiomba mahakama kutoa hati hizo kwa kuwa mshitakiwa na wadhamini wake hawajafika mahakamani bila kutoa taarifa.
 
Hakimu alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 4, mwaka huu, kesi itakapotajwa tena. Mujunangoma anadaiwa kupokea rushwa ya Sh milioni 323.4 kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana nje ya mahakama kutoka kwa watu wanaodai ni ndugu wa mshitakiwa, Mujunangoma alipata shinikizo la damu akiwa njiani kuja mahakamani hivyo alipelekwa katika Hospitali ya Arafa, Tabata, na kulazwa.
 
Ilidaiwa kuwa walitoa taarifa kwa mdhamini ili afike mahakamani kutoa taarifa lakini alichelewa na kukuta kesi imeshatajwa na hati hizo zimetolewa.
 
Mujunangoma anadaiwa Februari 5, 2014 katika Jengo la Benki ya Mkombozi, alipokea rushwa ya Sh milioni 323.4 kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya kufua Umeme ya VIP Engineering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalira.
 
Inadaiwa Mujunangoma, alipokea fedha hizo kupitia akaunti 00120102602001 kama tuzo baada ya kushughulikia masuala ya Kampuni ya IPTL kama mfilisi, bila kumtaarifu mkuu wake wa kazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.