AdSense

Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

Monday, 6 April 2015

On 05:24 by Unknown in    No comments
 
Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.


Akiongea  na  mwandishi wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.

“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye mitandao ya kijamii,  jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.

On 05:16 by Unknown in    No comments

Rapper Nay wa Mitego amesema amejiandaa kisaikolojia kupokea majibu ya kipimo cha DNA alichopima baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Siwema kugombana naye na kudai mtoto aliyezaa naye si wake.
Nay ameiambia Bongo5 kuwa bado zimebaki siku chache ili apewe majibu yake huku akidai kuwa amefanya hivyo ili kuandaa maisha ya mtoto wake ya baadaye.

“Mimi ni binadamu nimeshapitia mengi nilikotoka mpaka hapa nilipo na jibu lolote likija nitalikubali,”amesema.

“Kama sio mtoto wangu kama alivyosema basi nitamrudisha kwa baba yake japokuwa nitakuwa na maumivu lakini kuna wakati unaohitaji kufanya maamuzi magumu. Mimi sina ugomvi naye sema nimemchukua mwanangu baada ya kuona ana kazi nyingi. Nina imani huyu ni mwanangu hivi vingine vipo tu. Unajua hakuna mtu asiyefahamu kama Siwema ni mpenzi wangu na alivyovifanya kaamua tu na mimi nimeamua kwenda kupima DNA ili kumfanya mwanangu aishi maisha ya amani akikua, atajisikia vibaya akisikia huyo siy baba yako, lakini kama kutakuwa na vielelezo basi ni wazi atakuwa huru na amani,” ameongeza rapper huyo.

Kwa upande mwingine Nay alisema kuwa mgogoro huo umemharibia ratiba zake za muziki.

“Kama nilivyokuwa nimeahidi ninakuja tena na kazi mpya nikiwa na Diamond, hii sidhani kama itawezekana kwa sababu mimi nilingia kwenye matatizo ya kifamilia nikashindwa kufanya kazi zangu vizuri. Pia Diamond alikuwa anauguza, lakini nawaahidi mashabiki wa muziki wangu ndani ya wiki mbili nitaachia ngoma. Huenda ikawa ni hii ambayo nimefanya na Diamond au mimi mwenyewe au kolabo ya kimataifa. Ndani ya wiki hizi mbili kila kitu kitakuwa tayari.”

Sunday, 5 April 2015

On 19:32 by Unknown in    No comments
 
Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO'.
'Moyo' ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .
Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.
Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni 'single' ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.
Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi 'Usijali' akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.

On 19:31 by Unknown in    No comments
 
Mwanamama nguli na nyota wa kipindi cha runinga cha The Keeping Up with the Kardashians,Kim West ambaye ana mtoto mwenye umri wa miezi 21 North West aliyezaa na mumewe Kanye West,imeelezwa na mumewe huyo Kanye ,mkewe hataki chochote katika ulimwengu huu zaidi ya kupata mtoto mwingine ,lakini madaktari wamemuonya anaweza kukabiliwa na hatari kiafya.
Katika kipande cha kipindi kinachofuata cha kipindi cha mwanamama huyo ambacho kitarushwa katika runinga ya E’ inayojihusisha na masuala ya burudani na huenda kipande hicho kitarushwa mwishoni mwa wiki hii ,kipande hicho kinamuonesha Kim akielezea alichoambiwa na daktari wake kuwa anajaribu kumficha Kanye West anachotakiwa kwenda kufanyiwa na madaktari kuondoa kitu kilichoko kwenye kizazi chake.
Na ilipobidi kumkabili mumewe huyo, ambaye ni nguli wa muziki wa tambo,alipomwambia juu ya suala hilo tete, alikubaliana nalo na kumwambia endapo atafanikiwa kupata mtoto wa pili atakuwa wa mwisho kwasababu kondo la uzazi linakua kwenye kizazi chake.
 
lakini baadaye mrembo huyo alionekana kukata tamaa ya kupata mtoto mwingine,na akaeleza wazi kuwa alipokuwa mjamzito wa mtoto wao wa sasa North,alikuwa akiwaambia watu wake wa karibu kwamba hakuna kiwango cha pesa duniani atakachoweza kulipwa kurejea tena katika maumivu ya uchungu wa kuzaa.
Lakini,kwasasa hakuna kitu ninachokihitaji zaidi ulimwenguni kama kuwa mjamzito tena,nina pata hasira kidogo kwamba watoto wangu wataachana miaka kadhaa.
Siku za karibuni Kim alitoa ya moyoni kwa kueleza kwamba ulikuwa ni muujiza kuipata mimba ya mtoto wake North kwasababu madaktari walisha mwambia kuwa milele hataweza kubeba ujauzito .

Saturday, 4 April 2015

On 03:26 by Unknown in    No comments
 
HIVI NI KWAMBA MASTAA WAKIHISI KUWA HAWAONGELEWI NJIA PEKEE YA KURUDISHA UMAARUFU NI KUTUPIA PICHA ZISIZOKUWA NA MAADILI MTANDAONI?

HIVI PUNDE MSANII RECHO AMEWEKA PICHA AMBAZO KIUKWELI HAZINA MAADILI KWANI ZINAACHA SEHEMU KUBWA YA MWILI WAKE UKIWA HAUJAFUNIKWA KABISA, PICHA HIZO AMBAZO MAPAJA YOTE YAKO NJE ZIMEPONDWA SANA NA MASHABIKI AMBAO WAMEONYESHA KUTOKUBALIANA NAZO KABISA PICHA HIZO

 
DUUUH...HII NI LAANA KWELI. HIVI WANAFANYA MASHINDANO AU VIPI HAWA! 
On 03:21 by Unknown in    No comments
 

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.
 
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
 
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya.
 
“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond huku akiwataka Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
 
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga, aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni ya gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali.
On 03:07 by Unknown in    No comments
Kazi ipo! Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ juzikati alizua kizaazaa kisa ujauzito alipohudhuria kwenye msiba wa aliyekuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Taletale ‘Abdul Bonge’ aliyefariki dunia ghafla wikiendi iliyopita.


 Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari akifichwa na bodigadi wake.
Tukio hilo la Zari lilichukua nafasi katika Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo mkoani hapa ambapo mastaa kibao walisafiri kutoka Dar kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo.

ILIKUWAJE?
Awali, katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa mapema Jumanne wiki hii, Zari na Diamond, wakiwa wameongozana na wapambe wao walifika eneo la msiba ambapo kwa taratibu za Kiislam, wanawake hawachanganyiki na wanaume hivyo Zari akachukuliwa kwenda upande mwingine huku Diamond akielekea upande wa wanaume.

HALI YA HEWA YABADILIKA
Mara baada ya mastaa hao kutinga eneo hilo, umati mkubwa uliokuwa msibani hapo ulianza kuwazingira huku kila mmoja akitaka kuwaona. 


Akiingizwa garini.
 
ZARI AIBUA KIZAAZAA
Akiwa upande wa wanawake wenzake, Zari alijikuta akizungukwa na baadhi ya watu walionekana wazi kumchunguza kuanzia miguuni hadi kichwani ikidaiwa kuwa, walikuwa wakic
heki kama kweli ana mimba ya Diamond.

“Mwee, huyu ndiye Zari wa Diamond! Hivi mimba anayo kweli au ndiyo haya mambo ya mastaa wetu, mhh lakini kweli kitumbo kama kimetuna vile,” alisikika akisema mmoja wa wanawake hao.Uwepo wa mwanadada huyo uliwafanya wengi kusahau ishu ya msiba na kujikuta wakipigana vikumbo kumshangaa Zari ambaye muda mwingi alikuwa akijificha.

Kutokana na mazingira ya watu kukanyagana kutaka kumuona staa huyo, mrembo aliyefahamika kwa jina la Jestina George aligeuka kuwa bodigadi wake ili kumuepushia usumbufu ambapo alifanya kazi ya kumlinda.

PAPARAZI AZUIWA KUMPIGA PICHA
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
 “Weee, ukijaribu kupiga picha tunakorofishana, mwenyewe hataki kupiga picha, kama vipi nenda kamuombe ruhusa Diamond,” alisema Jestina huku akimficha Zari.
 Diamond akiimalisha usalama kwa mpenzi wake.
WATU WAANZA ZOGO
Kufuatia kitendo cha Jestina kumzuia mwandishi wetu kupiga picha, zogo lilianza eneo hilo huku baadhi ya watu wakihoji sababu za Zari kufichwa.“Au ni hiyo mimba yake ndiyo maana hamtaki apigwe picha? Acheni hizo bwana,” alisikika akiwaka kijana mmoja.

PAPARAZI AMFUATA DIAMOND
Baada ya paparazi kupigwa mkwara asipige picha alilazimika kwenda kumtafuta Diamond ili ampe ruhusa ya kwenda kumfotoa Zari lakini staa huyo naye alikataa na kueleza kuwa, kama anataka kufanya hivyo akachukue ruhusa kutoka kwa meneja wake.

Meneje huyo wa Diamond aliyefahamika kwa jina moja la Salam alipofuatwa alimruhusu paparazi kufanya kazi yake lakini aliporudi nyumbani palipokuwa na msiba kwa nia ya kumfotoa Zari, hali ilikuwa ileile hivyo kumsubiria mpaka Diamond alipotoka makaburini na alipofika kwenye gari lao, Zari alitolewa kwa kufichwa na Jestina kiasi cha kuwepo ugumu kupata sura yake.

 ZARI AINGIA KWENYE GARI FASTA
Huku watu wakimfuata kwa nyuma, Jestina alimchukua Zari na kumficha kwapani kisha kumkimbizia kwenye gari tayari kwa kuondoka eneo hilo.

DIAMOND NAYE APATA WAKATI MGUMU
Wakati Diamond akirejea kutoka makaburini, alijikuta akizingirwa na baadhi ya vijana ambao wengi wao hawajawahi kumuona ‘live’ hivyo kumpa wakati mgumu.Hata hivyo, ili kuwafurahisha, vijana hao walipata fursa ya kupiga naye stori mbili-tatu kabla ya kuondoka eneo hilo na kuacha umati ukiwasindikiza kwa macho.

Wednesday, 1 April 2015

On 10:12 by Unknown in    No comments
 
Picha  chafu  za  mwanadada  maarufu  nchini  Kenya, Risper  Faith  zimevuja  na  kusambaa  kwa  kasi  katika  mitandao  maarufu  ya  Kenya  na  Uganda.

Picha  hizo  ambazo  zinadaiwa  kusambazwa  na  mpenzi  wake  baada  ya  kuzinguana, zinamwonyesha  mwanadada  huyo  akiwa  ametunuka  huku  makalio  yake  na  mambo  mengine  adimu  yakiwa  hadhari  na  picha  nyingine  inaanika  kila  kitu  kama  alivyozaliwa.


Monday, 30 March 2015

On 19:18 by Unknown in    No comments

Yakatika na kuonyesha BACKYARD


Msamalia ajitokeza kumvalisha koti  
Tayari ndani  ya koti na kuendelea ku-perform
Lakini kumbe hayuko peke yake hata na wengine waliwahi kuumbuka
MINAJI
LADY GAGA
MOLLIE wa Chassing the Saturday
TOWIE



NAOMI CAMPBELL
On 18:49 by Unknown in    No comments
 
Lol......controversial Tanzanian singer and actress Baby Madaha says she has a problem of dreaming having sexy with a man who looks like Cristiano Ronaldo.
Speaking with Globalpublishers the scandalous celeb said she always gets that dream and it has reached a stage where she doesn't feel having a lover, According to Madaha she gets so tired when she wakes up in the morning because of that strange dreams.

"it is true mysterious romantic dreams disturbs me a lot, you can't believe I have been dreaming having sexy with a man who looks like Cristiano Ronaldo(international footballer palys for Real Madrid)" said Madaha

Sunday, 29 March 2015

On 20:49 by Unknown in    No comments
 
Ni hivi karibuni tu aliachana na mume wake, Nick Cannon baada ya kuishi kwa miaka sita lakini Mariah Carey hajataka kuruhusu matatizo yake binafsi yaathiri muziki wake na ndio maana yupo kwenye ziara barani Asia.

Muimbaji huyo mwenye miaka 44 Jumapili hii alikuwa na show huko Chengdu katika jimbo la Sichuan, China na kuwapa si tu burudani lakini pia kuwaonesha kufuli lake nje nje.

1413199097625_Image_galleryImage_Mandatory_Credit_Photo_by
1413199195946_Image_galleryImage_Mandatory_Credit_Photo_by

On 20:46 by Unknown in    No comments

Baada ya kuzaa tu hii ndio picha ya kwanza mwanadada Amber Rose kutupia  mtandaoni.
On 19:40 by Unknown in    No comments
 
Staa  wa  kike  anayetesa  katika  filamu  za  kibongo  Halima  Yahya  'Davina'  amefunguka  kuwa  mumewe  anamuonea  sana  wivu  kiasi  cha  kumfanya  ajihisi  kama  malkia  katika  ndoa  yao.

Akiteta  na  Mpekuzi, Davina  alisema: "Mume  wangu  ananionea  sana  wivu  hasa  siku  hizi  nilizojazia, lakini  wivu  wake  unaongeza  chachu  ya  mapenzi.

"Yaani  nikichelewa  kidogo  tu  anagomba  mpaka  baaasi.Lakini  kwangu  mimi  sioni  kama  ni  kero.Najisikia  furaha  kuona  nipo  na  mwanaume  anayenipenda  kwa  dhati."
On 19:38 by Unknown in    No comments
 
Lile sakata la mtoto kuwa si wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mujibu wa madai yaliyotolewa na mzazi mwenzake, Siwema limeingia hatua nyingine baada ya ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kusema majibu kamili ya kipimo cha vinasaba ‘DNA’ yatatolewa Aprili 8, mwaka huu.

Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, Nay alisema kila kitu kimekwenda sawa, hivyo anachosubiri ni hayo majibu ili ajue moja kwamba mtoto huyo mwenye miezi mitatu  ni wa nani kati yake yeye na mwanaume aliyetajwa na Siwema mwenyewe.
 
“Ndiyo natoka sasa kwenye ofisi ya mkemia. Hukumu ya DNA ile ni baada ya wiki mbili kuanzia leo (juzi Alhamisi). Lakini we acha tu. Mh! Nimeshafanya kila kitu, ni wao tu,” alisema Nay.
 
Aliongeza: “Ila mimi nashangaa. Yule mkemia aliyenipima, kaniambia, ‘Nay hukuwa na haja ya kupima DNA, mbona kwa uzoefu wetu hapa ukimwangalia mtoto anaonekana ni wako, ila kwa sababu umeamua kupima mwenyewe sawa.

“Nimeamua hivi ili mtoto aje kuwa na amani ukubwani, maana ujue atakapokua atakumbana na madai ya mama yake kwenye mitandao, sasa ni bora aje ajue ufumbuzi ulipatikanaje. Kama baba ni mimi au yule mzee anayemsema Siwema atajua.”
 
Mwandishi: “Hivi Nay, ikithibitika mtoto si wako utafanya nini?”
 
Nay: “Namrudisha kwa mama yake maana mimi nitakuwa baba haramu.”
 
Nay alisema siku ya kupima damu, alikwenda yeye na mtoto huyo ambapo walitumia dakika saba kutolewa damu kwa wote wawili. Bado mtoto huyo anaishi naye nyumbani kwake, Kimara, Dar.   

On 19:35 by Unknown in    No comments
HII ni habari ya kutisha! Takriban miaka mitatu imekatika tangu kifo cha aliyekuwa staa wa Bongo Movies, Steven Kanumba huku watu wawili wakifariki dunia kwa nyakati tofauti lakini nyuma ya pazia ya vifo vyao, mzimu wa Kanumba unatajwa kuhusika kutokana na watu hao kutaka kuishi mahali pa marehemu huyo.

Aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba.
Itakumbukwa kwamba, baada ya kifo cha Kanumba, mama yake mzazi, Flora Mtegoa ndiye aliyeshika jukumu la kusimamia mali za marehemu mtoto wake (alikuwa na haki).
Miongoni mwa mali hizo ukiachilia mbali, magari, vifaa vya kurekodia filamu, viwanja na filamu zilizokuwa hazijalipwa, mama Kanumba aliimiliki ofisi ya Kanumba iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Kanumba The Great Film iliyokuwa Sinza.Hata hivyo, hivi mapema Februari, mwaka huu, mama Kanumba alitoa vitu kwenye ofisi hiyo kwa madai ya kushindwa kulipa pango, hivyo ofisi ikawa wazi.

KILICHOTOKEA SASA
Habari ambazo gazeti hili ilizipata zilidai kwamba, mpangaji mwingine aliikodisha ofisi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini hivi karibuni mtu huyo amefariki dunia.Msikilize shuhuda: “Kuna jamaa alipanga kwenye ofisi iliyokuwa ya Kanumba mara tu baada ya mama Kanumba kuondoka vitu kwa kushindwa kulipia mkataba mpya.


“Huyo jamaa alikuwa anahusika na masuala ya ujenzi. Jamaa alilipia kodi ya mwaka mmoja, akawalipa watu wamfanyie usafi yeye akaenda ‘saiti’ kwenye mambo yake ya ujenzi. Inadaiwa akiwa kule, kuna ‘kijiko’  kilichokuwa kinachimba kiwanja, bahati mbaya kikarudi nyuma na kumgonga, akaanguka na kufariki dunia.”

JE, NI MZIMU WA KANUMBA?
Kifo cha mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, kinaunganishwa na tukio lilitokea mwaka juzi baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea  Aprili 7, mwaka 2012.Mara baada ya Kanumba kufariki dunia ghafla, mwanamke mmoja alikwenda kupanga nyumba ile aliyokuwa akiishi marehemu iliyopo Sinza, Dar, naye alifariki dunia ghafla.


MAJIRANI WALIZUNGUMZA
Wakati wa tukio hilo, wanahabari wetu walifika nyumbani kwa mwigizaji huyo ambapo walizungumza na majirani wakaelezea juu ya uwepo wa tukio hilo.Walisema japo hawaamini juu ya imani za masuala ya mzimu wa marehemu lakini kitendo cha mwanamke huyo kufariki dunia muda mfupi baada ya Kanumba kufa kiliwafanya washtuke na kuamini kwamba huenda ni mzimu wa Kanumba ndiyo ulichukua roho ya mpangaji huyo.


Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
WENGINE WALIAMINI HIVI
Hata hivyo, baadhi ya watu wengine pia walisema yao wakidai kwamba, wanaamini kifo cha mwanamke huyo ni cha kawaida kama ilivyo kwa vifo vingine.“Kama siku za Kanumba zilivyokuwa zimewadia na huyo mpangaji pia siku zake zilikuwa zimefika ndiyo maana amefariki dunia,” alisema mmoja wa majirani.


ALIVYOSEMA MZEE ALIYEKULA CHUMVI NYINGI
Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sumali (76), mkazi wa Mabibo-Relini, Dar akizungumza na gazeti hili kuhusu mazingira ya vifo hivyo, alisema:“Ipo mizimu ya hivyo. Mtu akifa, wa kwanza kuhamia kwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu naye anakufa. Lakini si kwamba nyumba ndiyo ina mizimu. Kama hivyo vifo vimetokea kweli basi na mzimu wa Kanumba umeshaondoka.”


MAMA KANUMBA AZUNGUMZA
Baada ya kuzipata habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya mama Kanumba kutaka kujua kama anajua lolote juu ya marehemu mtoto wake kuacha mzimu ambao unahusishwa na vifo hivyo ambapo alikiri kusikia taarifa za kifo cha jamaa aliyepanga kwenye ofisi za Kanumba lakini akasema hata yeye hajui sababu za kifo chake.


“Hata mimi nimesikia,  lakini sielewi chochote kuhusiana na mtu huyo kufariki dunia. Imenishtua kwa kweli maana si unakumbuka hata kule alikopanga (Kanumba) mwanzoni nako aliyepanga ile nyumba naye alifariki? Sijui hata ni kwa nini?” alihoji mama Kanumba kwa sauti iliyoashiria kushangaa sana.
On 19:33 by Unknown in    No comments

Uchuro? Baada ya kutundika mtandaoni kwa mara nyingine picha za jeneza alilojiandalia litakalotumika siku akiaga dunia, mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide, amelaaniwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho.

Mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide.
ABADILI RANGI
Mwaka 2012, Jide alitupia mtandaoni picha za jeneza lake lenye mchanganyiko wa rangi ya zambarau na nyeupe lakini safari hii amebadilisha na kutupia mengine mawili yenye rangi ya krimu na nyeupe.

MANENO KUNTU
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo anatumia jina la jidejaydee, juzi, mwanadada huyo, pamoja na picha hizo mbili, alisindikiza na maneno kuntu kwa chini yaliyosomeka, ‘Nimebadilisha mawazo yangu, sitaki tena lile la zambarau. Moja kati ya hayo hapo juu. Msinimaindi. Kila mtu atakufa. Nilikuwa nafikiria pia iwe kwa waalikwa tu. Sitaki kufunuliwa’.

MASHABIKI WAMLAANI
Risasi Jumamosi liliinyaka ishu hiyo sekunde chache baada ya Jide kuitupia ambapo ndani ya muda mfupi ‘posti’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ya kulaani kitendo hicho.
Baadhi ya mashabiki walieleza waziwazi kuchukizwa na jambo hilo alilolifanya staa wao wanayempenda.

SEHEMU YA MAONI
“Kifo kipo kwa kila binadamu lakini hatutakiwi kukifikiria hivyo dada (Jide) unamkosea muumba wako.
“Wewe ni kioo changu, ila kwa hili kwa kweli sijalipenda.
“Jamani dada mbona unatutisha au haupo sawa leo?
“Wewe wajina umefikiria nini lakini?
“Kama umeshaona unakufa sema tujue.

Muonekano wa jeneza hilo.
“Duh! Dada fanya maombi hiyo ni roho ya umauti.
“Dada nini tena mbona unamkufuru Mungu?                      Hata kama una machungu kiasi gani, huwezi kufanya hivyo kwani ni mipango ya Mungu. Muombe akusamehe.
“Wewe Jide wewe huogopi lakini?
“Najua sote tupo njia hiyo lakini kwa nini leo umeamua kutuandikia hivyo? Naomba mipango ya shetani ishindwe!” ilisomeka sehemu ya maoni hayo iliyoungwa mkono na baadhi ya mashabiki wake waliojawa na simanzi.

MCHUNGAJI AMUUNGA MKONO
Akizungumzia tukio hilo, mchungaji maarufu jijini Dar alisema kuwa, kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa kuwa kila nafsi itaonja umauti hivyo ni vema kujiandaa kwa kutenda mema.“Maandalizi yanayopaswa kuwa makubwa ni ya kiroho kwa kuhakikisha unatenda mema ili kupata tiketi ya kwenda peponi na kukwepa adhabu ya Jehanamu,” alisema mchungaji huyo.
On 19:32 by Unknown in    No comments
 
Msanii wa sinema za Kibongo, Ester Kiama.
Msanii wa sinema za Kibongo, Ester Kiama ametoa kioja cha aina yake baada ya kufunguka kuwa mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ ni mziba pancha wa magari yake ya kutembelea.

Akizungumza hivi karibuni na Global TV Online, Ester ambaye amekuwa akiandamwa kuwa huenda ana uhusiano wa kimapenzi na Dude ambaye ana mkewe, alisema hakuna chochote kinachoendelea kati yao zaidi ya kuwa mtu wake wa karibu na kumsaidia vitu vyake likiwemo suala la kuziba pancha.

Dude ndiyo kila kitu kwangu, ndiye anayeniendesha, ndiye anayenizibia pancha ikitokea dharura barabarani lakini pia mambo mengi tu yanayohusiana na filamu pamoja na binafsi,” alisema Ester.

Saturday, 21 March 2015

On 03:41 by Unknown in    No comments
 
 Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibu alijikuta akimwaga machozi baada ya kutembelea shule ya watoto wenye ulemavu ya Salvition Army, iliyopo Kurasini jijini Dar.
Staa huyo akiwa na timu yake ya Rozzie Magazine, walibeba misaada mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, maharage na sukari ambapo mara baada ya kufika kwenye ukumbi maalum uliotaarishwa kwa ajili ya kuzungumza na watoto hao, alishikwa na moyo wa huruma na kudondosha machozi.

Rose akiwa amebeba bidhaa kwa ajili ya walemavu.

“Kuna kitu nimejifunza hata kama hatuna tunahitaji kuja kuonana na watoto hawa kuzungumza nao na kuwafariji hivyo hata wasanii wenzangu wanapaswa kufanya hivi kwani ni muhimu katika maisha yetu,” alisema Rose.
On 03:40 by Unknown in    No comments
NYOTA wa filamu za Kibongo, Haji Adamu Rajabu ‘Baba Haji’ amefunguka kuwa, soko la filamu  Bongo kwa sasa linashuka siku hadi siku  na sababu kubwa ni  wasanii kutopenda kwenda shule kujiendeleza kielimu na kujua ni jinsi gani filamu inatakiwa kutengenezwa.
Nyota wa filamu za Kibongo, Haji Adamu Rajabu ‘Baba Haji’.
Akizungumza na Risasi Jumamosi,  Baba Haji alisema anakubaliana na kila mtu anayesema soko limeshuka kwa sababu wasanii wanapenda kukopi,  pia hawapendi kuandika miswada ya filamu na kupendelea kuingiza mambo ya kizungu, ingawa wengi wanamtaja msanii Steven  Kanumba kuwa ameondoka na soko hilo.

Baba haji anafunguka kama hivi…
Risasi Jumamosi: Vipi, mbona kimya kingi? Soko la filamu limekwenda na Kanumba au unalionaje?
Baba Haji: Tunaweza kusema hivyo, kwa sababu yeye alikuwa anajitoa kwa hali na mali, anatoa pesa zake kwa ajili ya filamu, ni tofauti na wasanii wengine ingawa pia alikuwa akitumia sana ‘media’ kueleza kila anachokifanya.

Risasi Jumamosi: Unadhani ni kwa nini wasanii wengi wanapenda kufanya kazi na Wanaigeria?
Baba Haji: Kwa sababu wao wanalipwa tu ila nchi nyingine wana sheria kali, kufanya kwao filamu ni mpaka uwe na digrii ya sanaa.

Risasi Jumamosi:  Wewe umejipanga vipi kwa hilo?
Baba Haji: Mimi nimejipanga vizuri kwa sababu nilikwenda Shule Bagamoyo (Pwani) kwa muda wa miaka mitatu na nilifanikiwa kupata diploma ya sanaa, wakati nakwenda shule nakumbuka Kanumba aliniambia napoteza muda kwani soko ndiyo lilikuwa limechanganya ila namshukuru Mungu hata niliporudi sijapotea sana kwa mashabiki.

Risasi Jumamosi: Una kipimo gani kinachoonesha hujapotea?
Baba Haji: Filamu nilizocheza ni nyingi na juzi nimegundua bado nipo baada ya filamu yangu ya Jamila na Pete ya Ajabu kutoka na kupokelewa na mashabiki vizuri mpaka wamelibadili jina langu kwa sasa wananiita Baba Jamila.

Risasi Jumamosi: Matarajio yako ya baadaye ni yapi?
Baba Haji: Mungu akipenda mwezi wa tisa narudi shule  kwa ajili ya kuchukua digrii ya sanaa ambayo nina uhakika itanipeleka mbali zaidi na nimefanikiwa kufungua kampuni yangu inayoitwa Hapa Production ambayo imeandaa filamu yangu ya kwanza ya Mama si Mama itatoka hivi karibuni Mungu akipenda.

Risasi Jumamosi: Unadhani ni kwa nini mnashindwa kupasua anga za kimataifa zaidi ukiacha ishu ya Kanumba kujitolea pesa zake mfukoni?Baba Haji: Nawashauri wasanii wajinoe zaidi kwenye lugha ya kigeni kwani na yenyewe inachangia wao kushindwa kufanya vizuri kwenye soko la kimataifa.

Marehemu Steven  Kanumba enzi za uhai wake.

Risasi Jumamosi: Unaweza kunipatia historia yako fupi ya sanaa tangu ulipoanzia mpaka sasa?
Baba Haji: Nilianza kuigiza 1998, nilianzia kundi lililoitwa Mtanzania ambalo lilikuwa chini ya Chama cha  Mapinduzi (CCM), mwaka 2000 nikaenda Nyota Academia kundi lililokuwa likiongozwa na mwalimu marehemu George Otieno ‘Tyson’, mkurugenzi akiwa ni Singo Mtambalike ‘Richie’.

Sikuishia hapo, mwaka 2002 tulianzisha Kundi la Kamanda Family nikiwa na Richie Mtambalike ambapo tulicheza michezo mbalimbali kisha tukaamua kuanza kucheza filamu ambapo tulicheza filamu ya Masaa 24 tukaona filamu ndiyo mpango mzima.

Mwaka 2003 nilicheza filamu ya Miss Bongo niliyoshirikiana na Aunt Ezekiel, iliyofuata ilikuwa ni Jeraha ya Ndoa, nilicheza na Monalisa.Mwaka 2004 nilikwenda Bukoba (Kagera) ambapo nilichukuliwa na Abantu Vision kwa ajili ya kufanya sinema iliyohusiana na mambo ya HIV ilivyoingia Tanzania. Filamu hiyo ilifanikiwa kuchukua Tuzo ya Ziff kama Filamu Bora ya mwaka 2005.

Mwaka 2010 nilijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambapo nilisoma mpaka kumaliza mwaka 2013.
Mwaka 2014 nilifanikiwa kucheza filamu nyingi kama vile Barbara, Kitoga, Don’t Cry, Mary Mary, Charles Mvuvi, Mwandishi wa Habari, Jamila na Pete ya Ajabu na Wa Mwisho Wewe.

Mwaka huu ndiyo wa mavuno kwangu kwani nimejiandaa vema kutoa filamu zangu mwenyewe ambazo zitakuwa na changamoto kubwa kwani nimesoma kwa ajili ya kuja kuvifanyia kazi na kuibadili kabisa tasnia ya filamu.
On 03:35 by Unknown in    No comments
Staa wa sinema  za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji Wastara Juma, Mark Edi.
Staa wa sinema  za Kibongo, Jacqueline Wolper.

Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.

“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.

Staa wa sinema  za Kibongo, Wastara Juma.
Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.

“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

Mwigizaji Wastara Juma, akiwa na mume wake mtarajiwa Mark Edi.
Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada zinaendelea.