AdSense

Monday, 6 April 2015

On 05:16 by Unknown in    No comments

Rapper Nay wa Mitego amesema amejiandaa kisaikolojia kupokea majibu ya kipimo cha DNA alichopima baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Siwema kugombana naye na kudai mtoto aliyezaa naye si wake.
Nay ameiambia Bongo5 kuwa bado zimebaki siku chache ili apewe majibu yake huku akidai kuwa amefanya hivyo ili kuandaa maisha ya mtoto wake ya baadaye.

“Mimi ni binadamu nimeshapitia mengi nilikotoka mpaka hapa nilipo na jibu lolote likija nitalikubali,”amesema.

“Kama sio mtoto wangu kama alivyosema basi nitamrudisha kwa baba yake japokuwa nitakuwa na maumivu lakini kuna wakati unaohitaji kufanya maamuzi magumu. Mimi sina ugomvi naye sema nimemchukua mwanangu baada ya kuona ana kazi nyingi. Nina imani huyu ni mwanangu hivi vingine vipo tu. Unajua hakuna mtu asiyefahamu kama Siwema ni mpenzi wangu na alivyovifanya kaamua tu na mimi nimeamua kwenda kupima DNA ili kumfanya mwanangu aishi maisha ya amani akikua, atajisikia vibaya akisikia huyo siy baba yako, lakini kama kutakuwa na vielelezo basi ni wazi atakuwa huru na amani,” ameongeza rapper huyo.

Kwa upande mwingine Nay alisema kuwa mgogoro huo umemharibia ratiba zake za muziki.

“Kama nilivyokuwa nimeahidi ninakuja tena na kazi mpya nikiwa na Diamond, hii sidhani kama itawezekana kwa sababu mimi nilingia kwenye matatizo ya kifamilia nikashindwa kufanya kazi zangu vizuri. Pia Diamond alikuwa anauguza, lakini nawaahidi mashabiki wa muziki wangu ndani ya wiki mbili nitaachia ngoma. Huenda ikawa ni hii ambayo nimefanya na Diamond au mimi mwenyewe au kolabo ya kimataifa. Ndani ya wiki hizi mbili kila kitu kitakuwa tayari.”

0 comments:

Post a Comment