Monday, 6 April 2015
On 05:20 by Unknown in HABARI No comments
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alihubiri akiwa
katika kiti cha magurudumu na kusema hawezi kuwatupa Mbunge wa Monduli
(CCM), Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa
kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi.
Pia
askofu huyo, amewataka waumini wote wa kanisa hilo kufika katika Kituo
Kikuu cha Polisi, Alhamisi ijayo siku ambayo atakwenda kukamilisha
mahojiano dhidi ya tuhuma za kumtukana Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar
es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.
Akihubiri
mamia ya waumini waliofika kanisani hapo kwa ajili ya ibada ya Pasaka
jana, Gwajima alisema kumekuwa na uvumi kwamba kuhojiwa kwake na polisi
kulitokana na kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa nyakati
tofauti na kuzungumza na waumini wake.
Alisema
alifahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 wakati huo mbunge huyo akiwa
Waziri wa Ardhi na tangu kipindi hicho amekuwa mtu wake wa karibu.
Alisema
alifahamiana na Dk Slaa tangu mwaka 1994 kabla hajagombea nafasi ya
urais kupitia Chadema na kwamba tangu wakati huo amekuwa rafiki wa
familia.
“Hawawezi
kunichagulia marafiki, hawa ni watu wangu wa karibu hata kabla hawajawa
na ndoto za kugombea urais, nitaendelea kuwa nao karibu,” alisema.
Asimulia mahojiano
Akizungumzia
mahojiano yake na polisi, Gwajima aliwaeleza waumini wake kwamba mambo
mengi aliyohojiwa hayakuhusiana na suala la kumkashifu Kardinali Pengo.
“Polisi
walinihoji mambo mengi binafsi yanayonihusu mimi na hayakuhusiana
kabisa na Pengo, maswali ya Pengo yalikuwa machache sana,” alisema.
Hata
hivyo, Gwajima alisema hana ugomvi na polisi wala Serikali kwa kuwa
amekuwa akitoa ushirikiano kwa vyombo hivyo. Akitoa mfano, alisema
Februari mwaka huu alipeleka barua polisi kueleza anataka kudhamini
kampeni kwa ajili ya kupinga mauaji ya albino kwa kushirikiana na jeshi
hilo.
“Niliwaeleza
kwamba tungezunguka na polisi mikoa yote Tanzania na wamenijibu kwamba
nipeleke ratiba ya shughuli hiyo ili tuanze,” alisema.
Alisema pia alidhamini mafunzo ya ulinzi shirikishi kwa vijana 400 kwa kushirikiana na polisi... “Shughuli
hizi zinaonyesha kwamba sina ugomvi na polisi, bali nimekuwa rafiki kwa
kushiriki katika shughuli zenye masilahi kwa Taifa.”
Viongozi wamiminika
Alisema pia hana ugomvi na Serikali na kwamba viongozi wake wamekuwa wakimiminika katika kanisa lake.
Aliwataja
viongozi hao kuwa ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa
Uchukuzi, Samuel Sitta, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison
Mwakyembe.
Viongozi
wengine, alisema ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye,
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee na wabunge wa Viti Maalumu, Dk
Mary Mwanjelwa na Vicky Kamata wote wa CCM
“Kama ningekuwa na ugomvi na Serikali viongozi hawa wasingekuja katika kanisa langu kwa nyakati tofauti. Hii inaonyesha nilivyo na uhusiano mzuri na Serikali,” alisema.
“Kama ningekuwa na ugomvi na Serikali viongozi hawa wasingekuja katika kanisa langu kwa nyakati tofauti. Hii inaonyesha nilivyo na uhusiano mzuri na Serikali,” alisema.
Alhamisi ijayo
Askofu Gwajima amewataka waumini wake kumsindikiza katika Kituo cha Polisi siku ambayo atahojiwa kwa mara nyingine. “Nitakwenda
Central Police Alhamisi saa moja asubuhi, nawaomba waumini wote mfike
katika eneo hilo lakini msilete fujo wala kumtukana mtu, kuweni watulivu
wakati wote nitakapokuwa nahojiwa,” alisema.
Askofu huyo alitakiwa kuhojiwa Alhamisi iliyopita lakini polisi waliahirisha kutokana na hali yake kutokuwa ya kuridhisha.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
alisema Jeshi la Polisi halitaruhusu mkusanyiko wa watu katika eneo hilo
wakati Askofu Gwajima atakapohojiwa.
“Atatakiwa
kufika na wakili wake na mtu mmoja ambaye ataona anafaa kuingia naye
kwenye mahojiano. Kama kuna waumini wanajiandaa kukusanyika katika ofisi
zetu hapa Central Polisi, wafahamu kwamba haturuhusu na wakikaidi
tutachukua hatua.”
Ilivyokuwa kanisani
Gwajima
alifika katika kanisa hilo lililopo kwenye viwanja vya Tanganyika
Packers Kawe saa 5.00 asubuhi na kupokewa kwa shangwe na waumini
walioanza kufika tangu saa 2.00 asubuhi.
Msafara
wa magari matatu; Toyota Land Cruiser mbili na Hammer, yaliwasili
kwenye viwanja vya kanisa hilo na kulakiwa na waumini walioyazingira kwa
shangwe na vigelegele wakitaka kumwona Askofu Gwajima.
Waumini hao walikuwa na shauku ya kumwona Gwajima na walionekana wakisukumana ovyo kila mmoja akitaka kumwona.
Akiwa
amevaa suti ya rangi ya kijivu na shati jekundu, Gwajima aliteremka
katika Hammer akishikiliwa na wasaidizi wake na kukalishwa katika kiti
cha magurudumu mawili kilichokuwa kikisukumwa na wasaidizi hao kuelekea
kwenye jukwaa la kanisa hilo.
Baada ya kufika, vikundi vya kwaya viliendelea kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali za kumtukuza Mungu.
Gwajima
alizungumza na waumini wake kuanzia saa 5.30 hadi saa 6.45, akiwaeleza
kilichotokea kuanzia siku alipofika polisi kwa mara kwanza, mahojiano
hadi alipotoka hospitali.
Katika mahubiri yake, Gwajima alisema ataendelea kuwaonya viongozi wa Serikali na wa dini watakaokosea masuala mbalimbali.
“Sitajali ni kiongozi wa aina gani amekosea nitawakemea. Rais akikosea nitamkemea. Waziri akikosea nitamkemea na viongozi wa dini wakikosea nitaendelea kuwakemea,” alisema.
“Sitajali ni kiongozi wa aina gani amekosea nitawakemea. Rais akikosea nitamkemea. Waziri akikosea nitamkemea na viongozi wa dini wakikosea nitaendelea kuwakemea,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Popular Posts
-
Iko hivi yani, Nimekua siwezi kujizuia hata kwa mwezi tu mmoja bila kutiwa na mwanaume yani mwanaume wangu, ikitokea nimeachana na ...
-
Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili: Mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwahiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujeng...
-
Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama mbili zil...
-
Wengine wanapenda sana wanawake wenye kina kirefu na wenginewenye kina kifupi. Hata hivyo, machaguo hayo huendana na urefu wa uume wa...
-
Basi kichwa cha mboo kikiwa juu ya kisimi chake alizidi kuhema kwa nguvu na mi bila huruma niliendelea kumsugua kisimi kwa kichwa cha mb...
-
Baada ya kukosa kazi katika sehemu za mambo ya massage kutokana umbile kubwa alilonalo hatimaye mwanamama huyu aja na mbinu kabambe ye...
-
Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mt...
0 comments:
Post a Comment