AdSense

Sunday 5 April 2015

On 19:38 by Unknown in    No comments
 
Shirikisho la soka barani Africa CAF limethibitisha kuwa Morocco itashiriki katika mechi za kufuzu kwa dimba la Afrika mwaka 2017.
Siku ya alhamisi mahakama ya kusuluhisha mizozo ya michezo Cas ilibadilisha marufuku iliowekwa na CAF dhidi ya Morrocco ya kutoshiriki michuano ya mwaka 2017 na 2019.
Lakini siku ya ijumaa mkurugenzi wa mawasiliano wa CAF Junior Binyam aliiambia BBC kwamba kuna mikutano mingi itakayofanywa kabla ya uamuzi kufanywa.
''Tusubiri kitakachofanyika'',alisema.Droo ya mechi za kufuzu inatarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi Aprili.
Siku ya jumapili,Shirikisho la soka barani CAF lilitanagaza kuwa lilikubali uamuzi uliofanywa na mahakama hiyo kufuatia mkutano mkuu wa kamati ya mahakama hiyo huku ikitoa sababu zao katika mtandao.

0 comments:

Post a Comment