Thursday, 9 April 2015
On 21:22 by Unknown in SIASA No comments
Akihubiri
siku ya Pasaka katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo
Mwenge katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe alisema
kwamba, inajulikana wazi kwamba Lowassa amekuwa anautaka Urais kwa udi
na uvumba kwa miaka mingi, hata mwaka 1995 alijitosa hadharani kuuwania,
sasa anapodai kwamba hivi sasa kuna makundi yanayokwenda kwake
kumshawishi agombee Urais, kana kwamba yeye hataki Urais, anakuwa
anamdanganya nani?
Ingawa katika mahubiri hayo ya saa mbili, Kakobe hakumtaja Lowassa kwa jina, hata hivyo Kakobe alisema, "Wako
watu wengine ambao inajulikana wazi kwamba wamekuwa wakiutaka Urais kwa
udi na uvumba, kwa miaka mingi, lakini hivi sasa wanasema kuna makundi
ya watu yanawafuata nyumbani, kuwashawishi kugombea Urais; kama vile
hawautaki Urais, hivi watu hawa wanamdanganya nani?
"Na
wale wanaokwenda kumshawishi mtu ambaye kwa miaka mingi, anajulikana
kwamba anautaka Urais, hawajui kwamba nao wanafanywa kuwa wajinga? Mtu
anayejulikana kwa muda mrefu kwamba anautaka Urais, ni vema akatangaza
tu moja kwa moja nia yake, bila haja ya ghiliba."
Katika
mahubiri yake yenye kichwa, "UPOTOSHAJI WA UKWELI", Kakobe alieleza
jinsi Gavana wa Kirumi, au liwali Pontio Pilato, alivyojiunga na
Viongozi wengine kupotosha ukweli wa kufufuka kwa Yesu, na kusema kwamba
wanafunzi wake waliuiba mwili wake, wakati askari walinzi walipokuwa
wamelala, na kuwadanganya watu, ingawa wao wenyewe waliujua ukweli.
"Pilato
aliwadanganya watu hao kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli ulikuwa
dhahiri, walipomwona Yesu kati yao kwa muda wa siku 40. Unaweza
kuwadanganya watu kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli hudhihirika, na
kumfedhehesha yule aliyeupotosha ukweli huo", alisema.
Aliendelea
kusema kuwa, hata leo kuna upotoshaji wa kweli mbalimbali za kiroho na
kimwili. Baada ya kuelezea juu ya baadhi ya kweli za kiroho
zilizopotoshwa, aliwageukia wanasiasa waongo, akianza kwa kutoa mfano wa
Waziri wa Habari wa Iraq, wakati wa vita ya mwaka 2003, Muhammad Saeed
al-Sahhaf, aliyekuwa akipotosha ukweli kuhusu jinsi Iraq ilivyokuwa
inapigwa vibaya katika vita hivyo, na akaendelea kusema;
"Kabla
sijaendelea, nifafanue kwanza juu ya watu wanaopotosha ukweli, kwa
kusema kwamba eti Wachungaji hawapaswi kuwakemea wanasiasa
wananapopotoka. Watu hawa hawajui Biblia. Katika MAMBO YA WALAWI
4:22-23, Biblia inasema, Mtawala akifanya dhambi, inampasa Kuhani yaani
Mchungaji, kumjulisha dhambi yake."
Kakobe
aliendelea kusema kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo Watanzania
wawe makini na wanasiasa waongo wanaofanya uongo kuwa sehemu ya siasa
zao.
"Siasa,
ni Sayansi, inaitwa POLITICAL SCIENCE, na "any kind of science only
deals with facts". Wanasiasa hawana budi kuwa wakweli kwa kuwa siasa ni
sayansi.
"Siasa
siyo mchezo mchafu, bali baadhi ya wanasiasa ndiyo wachafu.
Msidanganywe tena na wanasiasa ambao watakuja kwenu mwaka huu na ahadi
za uongo za kuibadili miji na kuifanya kuwa kama New York, kwa miaka
mitano; na wengine hawana AIBU, wanaweza hata kuwaambia wakazi wa Dodoma
kwamba watawaletea meli! Hamna budi kuyachunguza kwa makini maneno yao,
na kuona kama ni ya kweli."
Kuhusu
Katiba, Kakobe aliwaunga mkono Maaskofu waliowapa Wakristo maelekezo ya
kuikataa Katiba Pendekezwa, katika Kura ya Maoni, na kusema kwamba hiyo
ndiyo kazi ya Mchungaji.
"Mchungaji,
pia ni Mwalimu, kazi yake ni kuchunga na pia kulisha kondoo (YOHANA
21:15-17), na Biblia inafafanua juu ya kazi ya Mwalimu katika ISAYA
30:20-21, ikieleza kwamba Mwalimu anatakiwa kuwaambia anaowaongoza,
"Njia ni hii ifuateni, wageukapo kwenda kulia au kushoto".
Aliendelea kusema, "Kumekuwa
na udanganyifu au upotoshaji wa ukweli kuhusu Katiba, tangu katika
hatua za mwanzo kabisa za mchakato wa Katiba, ambapo Chama kimoja cha
siasa, kiliwapachika makada wake katika vikundi mbalimbali, ili kiwe na
wajumbe wengi.
"Kwa
mfano Kingunge Ngombale Mwiru aliwawakilisha waganga wa kienyeji,
lakini cha ajabu, ukienda kwake hata leo, hakuna kibao kwake
kinachozitambulisha kazi zake za uganga wa kienyeji, kama ilivyo kwa
waganga wengine! Siyo hilo tu, kote duniani, Katiba yoyote ya nchi,
lazima itokane na muafaka wa Kitaifa, ili Katiba hiyo iwe na sifa ya
kusomeka katika Utangulizi wake, "SISI WANANCHI".
"Hapa
kwetu, watawala hawakutaka kabisa muafaka katika kutengeneza Katiba
yetu, lakini wanadai eti, Katiba Pendekezwa, ni bora kuliko zote Afrika!
Huu ni upotoshaji wa ukweli, wa hali ya juu sana."
Aliendelea
kusema kwamba, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Kura ya
Maoni, hazikuzingatiwa kikamilifu katika mchakato huo uliojaa
udanganyifu.
"Sheria
ya Kura ya Maoni, Ibara ya 5(3), inasema kwamba kungetakiwa kuwepo na
elimu kwa wapiga kura, kwa siku 60, mara tu baada ya Tangazo la Katiba
Pendekezwa katika Gazeti la Serikali Na. 382 lililotolewa tarehe
10.10.2014, lakini elimu hiyo iliyopaswa kutolewa na Tume ya Uchaguzi,
haijafanyika hadi hivi leo!
V"ilevile,
Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 4(3) na 4(4), inasema kwamba
kungetakiwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali, SWALI LA KURA YA
MAONI, ambalo wananchi wangelijibu kwa jibu la NDIYO au HAPANA, na pia
Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 12(1) na 12(2) na Ibara ya 16(1)
inasema kwamba, kungetakiwa kuwepo na Kamati mbili za Kura ya Maoni,
Kamati moja ya NDIYO, na nyingine ya HAPANA, ambazo zingejumuisha
wananchi wenye misimamo tofauti kutoka katika makundi mbalimbali katika
jamii, na Kamati hizo zingepiga kampeni kwa siku 30.
"Yote
haya hayakuzingatiwa, lakini kinyume chake, Watawala hadi hivi leo,
hawataki hata kusikia watu wakisema HAPANA kwa Kura ya Maoni, na wakati
huohuo, wengine bado wanataka Kura ya Maoni ifanyike Aprili 30, pamoja
na kwamba imetangazwa na Tume ya Uchaguzi, kwamba imeahirishwa!
"Wachungaji
wengine wenye njaa, wanathubutu kusema kwamba eti kwa sababu kwenye
Katiba Pendekezwa kuna Uhuru wa kuabudu, basi sisi Wachungaji tukae
kimya, mengine hayatuhusu, hawa wana njaa kali, na upeo mdogo wa uelewa
wa mambo haya.
"Mimi
sina njaa, na ninasema kwa msisitizo, Katiba ni zaidi ya Uhuru wa
kuabudu. Ilikuwa rahisi kwa Pilato kuwadanganya watu wa nyakati hizo,
lakini leo ni kazi sana kuwadanganya watu wanaopata maarifa na habari
juu ya yote yanayofanyika kote duniani, kwa TV, Redio, Magazeti,
Intaneti na Mitandao ya kijamii.
"Watu
wanajua kwamba kote ulimwenguni, Katiba ya Wananchi hutokana na
muafaka, na Kura ya Maoni, hufanyika baada ya Kampeni ya NDIYO na
HAPANA, kama ilivyofanyika Kenya ambako waliosema NDIYO waliitwa kundi
la NDIZI, na waliosema HAPANA waliitwa kundi la CHUNGWA.
"Waliowaambia
Wakristo wapige kura ya HAPANA kwenye Kura ya Maoni, ninawapa asilimia
90, hata hivyo kwa unyenyekevu, mimi ninaomba kuhitilafiana nao, kwa
kuongeza kwamba Kura ya Maoni inapaswa kususiwa kabisa, kwa sababu
kushiriki katika Kura hiyo, ni kuuhalalisha udanganyifu wa Watawala
hawa, na kujifedhehesha mwishoni.
"Tangu
mwanzo, watu hawa walitumia ubabe na wizi wa kura wa dhahiri katika
Bunge la Katiba, na kutangaza kura feki za NDIYO za mahujaji na wajumbe
wengine ambao hawakuwepo ukumbini wakati wa kupiga kura, na pia kura za
Wazanzibari feki, na hivyo kupitisha kwa lazima, Katiba Pendekezwa.
"Wamedhamiria
kufanya hivyohivyo hata katika Kura ya Maoni, ili kuipitisha kwa lazima
Katiba yao Pendekezwa; ukizingatia kwamba, ili kutimiza kusudi hilo,
wameweka sheria mbaya kwa makusudi ya kuhalalisha udanganyifu.
"Kwa
mfano Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 34(2), inahalalisha wapiga kura
walioandikishwa Tanzania Bara, kwenda kupiga kupiga Kura ya Maoni, huko
Zanzibar. Katika mazingira haya, Kura za HAPANA zitasaidia nini? Ni
kuhalalisha tu udanganyifu wao, na kujifedhehesha.
"Mwandishi Mkuu wa Katiba Pendekezwa, yeye mwenyewe amesema anapenda aitwe JOKA LA MAKENGEZA! Niliposikia juu ya Jina lake hili, nilipigwa na butwaa!
Katika Biblia, Joka ni Ibilisi au Shetani (UFUNUO
12:7-9; 20:1-2), maana yake ni kwamba Mwandishi Mkuu wa Katiba
Pendekezwa, ni Joka yaani Shetani, na hivyo tunaweza kusema Katiba hiyo
ni ya Kishetani, maana imetokana na Shetani ambaye ni Joka lililoko
kuzimu!
"Kumbe basi, siyo tu kwamba Katiba Pendekezwa imeahirishwa, ila ni kwamba Mungu ameikataa tangu siku ya kwanza ya mchakato wake!
"Kwa
sasa tuwaze tu kujiandikisha kwa wingi katika Uandikishaji wa Wapiga
Kura, kwa BVR, na kuwa tayari tu kwa Uchaguzi Mkuu, na kuisahau kabisa
Kura ya Maoni."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Popular Posts
-
Iko hivi yani, Nimekua siwezi kujizuia hata kwa mwezi tu mmoja bila kutiwa na mwanaume yani mwanaume wangu, ikitokea nimeachana na ...
-
Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili: Mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwahiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujeng...
-
Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama mbili zil...
-
Wengine wanapenda sana wanawake wenye kina kirefu na wenginewenye kina kifupi. Hata hivyo, machaguo hayo huendana na urefu wa uume wa...
-
Basi kichwa cha mboo kikiwa juu ya kisimi chake alizidi kuhema kwa nguvu na mi bila huruma niliendelea kumsugua kisimi kwa kichwa cha mb...
-
Baada ya kukosa kazi katika sehemu za mambo ya massage kutokana umbile kubwa alilonalo hatimaye mwanamama huyu aja na mbinu kabambe ye...
-
Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mt...
0 comments:
Post a Comment