AdSense

Saturday, 21 March 2015

On 03:41 by Unknown in    No comments
 
 Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibu alijikuta akimwaga machozi baada ya kutembelea shule ya watoto wenye ulemavu ya Salvition Army, iliyopo Kurasini jijini Dar.
Staa huyo akiwa na timu yake ya Rozzie Magazine, walibeba misaada mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, maharage na sukari ambapo mara baada ya kufika kwenye ukumbi maalum uliotaarishwa kwa ajili ya kuzungumza na watoto hao, alishikwa na moyo wa huruma na kudondosha machozi.

Rose akiwa amebeba bidhaa kwa ajili ya walemavu.

“Kuna kitu nimejifunza hata kama hatuna tunahitaji kuja kuonana na watoto hawa kuzungumza nao na kuwafariji hivyo hata wasanii wenzangu wanapaswa kufanya hivi kwani ni muhimu katika maisha yetu,” alisema Rose.

0 comments:

Post a Comment