Thursday, 9 April 2015
On 21:17 by Unknown in SIASA No comments

Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi
ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama
hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Zitto
ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama
wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema,
ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata
usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.
Pia,
amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma,
akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni
lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga
kuyabeba majimbo yote.
Akizungumza na Gazeti la
Mwananchi jijini Dar es Salaam, Zitto alisema
ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano
wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na
kufanya uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho
kinaungwa mkono na watu wengi.
“Tuna wagombea ubunge
wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba
hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata
katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya uamuzi,” alisema.
Huku
akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema wabunge hao ndiyo sababu ya
chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na kufafanua kuwa ACT
kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama vya Chadema na CCM.
“Wale
ambao wanabanwa CCM na kukosa uhuru wa kuhoji jambo lolote hiki (ACT)
ndicho chama chao. Wale ambao wanaamini kuwa aina za siasa tulizotaka
kuzifanya ndani ya Chadema tukashindwa kuzifanya na wanadhani ni siasa
muhimu zinazotakiwa, wapo na sisi,” alisema.
Kuhusu Kigoma
“Nahitaji
majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili
hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa
anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” alisema Zitto ambaye pia
alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini
siyo Kigoma Kaskazini.
Kauli hiyo ya Zitto inawagusa
wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali
(Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu
Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na
Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert
Obama (Manyovu) wa CCM.
Alipoulizwa iwapo wabunge hao
wa majimbo ya mkoa huo ni miongoni mwa watu watakaohamia chama hicho
alisema, “Sasa huo ni mtizamo wenu. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe na
msingi, nataka msingi uwe Kigoma.
"Tutakutana tena
kwenye chumba hiki (cha mikutano) baadaye mwezi Novemba ili mnisute kwa
kauli yangu na hapo itakuwa baada ya matokeo kutoka. Nahitaji kushinda
kila kitu."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Popular Posts
-
Iko hivi yani, Nimekua siwezi kujizuia hata kwa mwezi tu mmoja bila kutiwa na mwanaume yani mwanaume wangu, ikitokea nimeachana na ...
-
Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili: Mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwahiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujeng...
-
Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama mbili zil...
-
Basi kichwa cha mboo kikiwa juu ya kisimi chake alizidi kuhema kwa nguvu na mi bila huruma niliendelea kumsugua kisimi kwa kichwa cha mb...
-
Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mt...
-
Wengine wanapenda sana wanawake wenye kina kirefu na wenginewenye kina kifupi. Hata hivyo, machaguo hayo huendana na urefu wa uume wa...
-
Baada ya kukosa kazi katika sehemu za mambo ya massage kutokana umbile kubwa alilonalo hatimaye mwanamama huyu aja na mbinu kabambe ye...
-
No.1. Jennifer Lopez Anautajiri wa dola milioni $250 ,jinsi gani alipata hu utajiri,?? Nikutokana na uigizaji wake, Mfanyabiashara na ...
0 comments:
Post a Comment