AdSense

Monday, 6 April 2015

On 05:24 by Unknown in    No comments
 
Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.


Akiongea  na  mwandishi wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.

“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye mitandao ya kijamii,  jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.

0 comments:

Post a Comment