Saturday, 21 March 2015
On 03:35 by Unknown in WASANII No comments
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na
tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji
Wastara Juma, Mark Edi.
Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye
maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha
uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini
alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.
“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha
Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wetu alimtafuta Mark ili
kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na
kudai amemchoka mwigizaji huyo.
“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

Jitihada za kumpata Wolper ili aweze kufunguka kwa upande wake
hazikuzaa matunda kwani simu yake iliita bila kupokelewa, jitihada
zinaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment