AdSense

Friday, 20 March 2015

On 18:59 by Unknown in    No comments
Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota hivi karibuni alipoteza fahamu baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Gharibu Dumba.
Salma Dakota Akionyeshwa pete aliyovishwa.

Tukio hilo lilitokea kwenye Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda bila kujua kuwa mtu wake huyo alikuwa na jambo kubwa la kumfanyia.
Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile, alishangaa akivishwa pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo gharama yake ni takriban shilingi milioni 3.

Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota akiwa kwenye pozi.

Akizungumzia tukio hilo mtangazaji huyo alisema: “Nilipata mshituko kwani sikutarajia na ndiyo maana nikapatwa na hali ile. Namshukuru Mungu kwa hili lililonitokea, ni jambo la heri na Mungu aniongoze katika safari hii ya kuelekea kwenye maisha ya ndoa.”

0 comments:

Post a Comment