AdSense

Sunday, 29 March 2015

On 19:32 by Unknown in    No comments
 
Msanii wa sinema za Kibongo, Ester Kiama.
Msanii wa sinema za Kibongo, Ester Kiama ametoa kioja cha aina yake baada ya kufunguka kuwa mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ ni mziba pancha wa magari yake ya kutembelea.

Akizungumza hivi karibuni na Global TV Online, Ester ambaye amekuwa akiandamwa kuwa huenda ana uhusiano wa kimapenzi na Dude ambaye ana mkewe, alisema hakuna chochote kinachoendelea kati yao zaidi ya kuwa mtu wake wa karibu na kumsaidia vitu vyake likiwemo suala la kuziba pancha.

Dude ndiyo kila kitu kwangu, ndiye anayeniendesha, ndiye anayenizibia pancha ikitokea dharura barabarani lakini pia mambo mengi tu yanayohusiana na filamu pamoja na binafsi,” alisema Ester.

0 comments:

Post a Comment